Zijue faida za kufanya mazoezi kila siku



Mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwa afya yako, kuna namna mbalimbali za kufanya mazoezi, Unaweza kufanya mazoezi ya viungo fulani vya mwili wako kama miguu, mikono, mgongo. 

Kuna mazoezi ambayo ukifanya utakuwa umefanya zoezi lilojumuisha kiungo zaidi ya kimoja mfano mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba na mengineyo.
Unaweza kutumia muda kidogo kufanya mazoezi kwa takribani dakika (30-45) kwa siku iwe asubuhi au jioni unaweza kupata faida nyingi za kiafya kwa kufanya mazoezi hayo.
Kuna faida nyingi za kufanya mazoezi, leo tumekuletea 12 zenye  manufaa na ufahamu wa afya yako.
1. Mazoezi huboresha ufahamu wako uwezo wa kuelewa na kufikiri mambo katika mazingira yanayokuzunguka.
2. Mazoezi hukufanya uchangamke na kuwa shupavu.
3. Mazoezi husaidia kupunguza msongo wa mawazo.
4. Mazoezi huboresha uwezo wako wa kuhifadhi kumbukumbu.
5. Mazoezi humfanya mtu ajiamini.
6. Mazoezi huimarisha moyo hivyo hukuepusha na maradhi mengi yatokanayo na mapigo mabaya ya moyo.
7. Mazoezi husaidia kuweka sawa kiwango cha cholesterol au mafuta yaliyopo mwilini.
8. Mazoezi hupasha mwili joto hivyo husaidia kuzuia baridi.
9. Mazoezi hushusha kupanda kwa shinikizo la damu. (high blood pressure)
Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata baadhi ya maradhi ya saratani.
10.Mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kisukari.
11. Mazoezi humsaidia mtu kuondokana na baadhi ya matatizo ya akili.
12. Mazoezi hupunguza uzito wa ziada wa mwili na kufanya mwili wako kuwa mwepesi.

Hizo ni baadhi ya faida za kufanya mazoezi, yote ya yote kufanya mazoezi hufanya uwe mwenye afya njema.
Ni vyema ukajiuliza, hivi ni kweli ukifanya mazoezi na kula vyakula bora kunaweza kuboresha maisha yako? Jibu ni NDIYO mazoezi na vyakula ni dawa pekee ya kutibu au kukuepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika.

Post a Comment

Previous Post Next Post