DC na Mbunge Jimbo la Kilindi, Tanga waungana matembezi kuhamasisha Sensa



Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Yeji Busalana siku ya leo na Mbunge wa Jimbo la Kilindi Omar Kigua wameongoza maandamano ya kuhamasisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika tarehe agosti 23, 2022. Katika kuhitimisha matembezi hayo katika viwanja vya shule ya sekondari SEUTA  Matembezi hayo Mbunge aliwahimiza wananchi wa Jimbo la Kilindi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu zoezi la sensa ya watu na makazi ili serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan iweze kuwawekea mipango bora ya maendeleo yao.





Naye Mkuu wa Wilaya aliwaeleza wananchi kuwa maendeleo yote wanayoyaona yanaweza kufanyika zaidi endapo serikali itakuwa na takwimu sahihi za idadi ya wananchi waliopo wilayani Kilindi kwa ajili ya kuwaletea huduma za jamii kama elimu, afya, miundombinu ya barabara na maji na kuwataka kuwapa ushirikiano makarani watakaofika maeneo yao kwa kutoa taarifa za kweli.

Kwa nyakati tofauti Mbunge na Mkuu wa Wilaya walimshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuiletea wilaya ya Kilindi maendeleo kila siku na kusema kuwa ujenzi wa barabara ya Handeni hadi Singida kupitia Wilaya ya Kilindi itaifungua wilaya ya Kilindi na kuleta maendeleo makubwa.

Katibu Tawala Wilaya ya Kilindi akifurahia mashindano ya uvutaji kamba

Matembezi hayo pia yaliambatana na burudani mbalimbali na zawadi kwa washiriki wa mashindano yaliyofanyika zilitolewa.

Post a Comment

Previous Post Next Post