Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilindi yapatiwa Milioni 100 ujenzi wa bwalo la chakula

Tatizo la ukosefu wa bwalo la chakula katika sekondari ya wasichana Kilindi limepatiwa ufumbuzi baada ya serikali kuu kutoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa bwalo


Akizungumza ofisini kwake kuhusu fedha hizo Afisa Elimu sekondari wilaya Kilindi ndg Ntuli A.Mwakabungu amesema ujenzi wa bwalo hilo katika shule hiyo ya bweni ni mikakati ya serikali kuhakikisha miundombinu ya elimu inajengwa ili kuboresha mazingira ya elimu wilayani Kilindi

Amesema ujenzi wa bwalo hilo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba,2022

Bwana Mwakabungu amesema idara ya elimu sekondari kwa namna ya kipekee inatoa shukrani kwa Mh: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa bwalo hilo.

Amesema tayari mchanga, saruji na mawe kwa ajili ya ujenzi wa msingi vimeshawekwa eneo la mradi.

Pia amesema serikali kuu imetoa kiasi kingine Cha fedha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Pagwi

Amesema ujenzi wa nyumba hiyo pia unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba,2022

Amesema ujenzi wa nyumba hii ambayo itatumiwa na walimu 2 itapunguza tatizo la ukosefu wa nyumba hizo na kulingana na mahitaji shule itakuwa na inahitaji nyumba 8 na kutoa shukrani kwa serikali kusaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa nyumba za walimu

Shule ya sekondari Pagwi kwa sasa ina wanafuzi 286 na walimu 11
Modi Mngumi

Post a Comment

Previous Post Next Post